Rais john magufuli amelipongeza shirika la utangazaji tanzania – TBC kwa kuandaa vipindi ambavyo vimekuwa vikitoa suluhisho la matatizo yanayowakabili wananchi hasa wale wa vijijini.
Rais magufuli ametoa pongezi hizo ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na wakazi wawili wa mkoa wa njombe wanaozalisha umeme kwa njia ya maji na kuwasambazia wakazi wenzao.
Wakati wa mkutano huo, Rais MAGUFULI ameliagiza Shirika la Umeme Nchini – TANESCO, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na viongozi Wakuu wa Wizara ya Maji kwenda mkoani NJOMBE kwa lengo la kuwasaidia Wakazi hao ili waweze kuzalisha umeme mwingi zaidi.