Rais: Haki iliyocheleweshwa ni haki iliyonyimwa

0
171

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa haki ndiyo msingi wa maendeleo katika Taifa lolote duniani.

Rais amesema hayo mara baada ya kuwaapisha Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani aliowateua hivi karibuni huku akiwataka kwenda kufanya kazi kwa bidii kwani haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyonyimwa.

Ameeleza kuwa katika utendaji wao wafahamu kuwa sheria, kanuni na miomgozo yote inachangia tu asilimia 70, huku asilimia 30 ikitokana na nafasi na utu wao.

Ametumia jukwaa hilo kuupongeza mhimili wa mahakama kwa kazi nzuri unayofanya licha ya changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili kama vile kukosekana vitendea kazi vya kutosha, uchakavu wa majengo, kutokuwepo mahakimu wa kutosha na maslahi ya watumishi.

Hata hivyo ameahidi kuwa serikali itaendelea kutatua changamoto hizo kadiri muda na uwezo utakavyoruhusu.