Rais Dkt Magufuli kuwaapisha viongozi wapya Februari 3

0
424
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli

Rais Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 03 Februari, 2020 atawaapisha viongozi wa wizara, mahakama, majeshi na mikoa aliowateua juzi kushika nyadhifa mbalimbali.

Viongozi watakaoapishwa ni makatibu wakuu watano, naibu katibu mkuu mmoja, makatibu tawala wa mikoa mitatu, kamishna Jenerali wa Magereza na Kamishna jenerali wa zimamoto na uokoaji.

Wengine ni kamishna wa ardhi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, msajili mkuu wa mahakama ya Tanzania, msajili wa mahakama ya rufani, msajili wa mahakama kuu na wajumbe watatu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Viongozi hao wataapishwa kuanzia saa 3:15 asubuhi, Ikulu Jijini Dar es Salaam na wanatakiwa kufikia Ikulu kabla saa 2:00 asubuhi kupitia lango la Mashariki (Lango la Baharini).