Rais Dkt. John Magufuli amewaapisha Mabalozi

0
197

Rais Dkt. John Magufuli amewaapisha Mabalozi aliowateua hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania katika mataifa ya Afrika Kusini, Namibia, Zimbabwe, na Nigeria.

Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi ameapishwa kuwa Balozi wa
Tanzania Nchini Afrika Kusini, Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa
Balozi wa Tanzania Nchini Namibia, Profesa Emmanuel Mwaluko Mbennah
kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe na Dkt. Benson Bana kuwa
Balozi Tanzania Nchini Nigeria.