Rais Atuma Salamu za Pole Kifo cha Augustino Mrema

0
178

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa familia na wanachama wa chama cha TLP, kufuatia kifo cha mwenyekiti wa chama hicho Augustino Mrema kilichotokea leo asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo mkoani Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia amesema atamkumbuka Mrema katika mchango wake kwenye mageuzi ya siasa, uzalendo na upendo kwa Watanzania.