Rais Samia ametuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na Waandishi wa habari, kufuatia ajali ya gari iliyotokea wilayani Busega mkoani Simiyu na kusababisha vifo vya watu 14 wakiwemo Waandishi wa habari sita,
Katika salamu alizozituma kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia Suluhu Hassan amesema ameshtushwa na ajali hiyo na ameomba kwa Mwenyezi Mungu aziweke mahali pema roho za marehemu.
Kwa upande wa majeruhi, amewaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka.
Ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha Shimanyire, imehusisha gari lililokuwa katika msafara wa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ambaye alikuwa akielekea wilayani Ukerewe, na limegongana uso kwa uso na gari ndogo ya abiria aina ya Hiace.