Rais atoa pole kwa familia ya Mwinyi

0
323

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia kifo cha Hassan Ali Hassan Mwinyi ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan mwinyi, na Kaka wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi.

Katika salamu zake za pole alizozitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia Suluhu Hassan amesema anaipa pole familia ya Mzee Mwinyi kufuatia msiba huo.