Rais atia saini miswada miwili kuwa sheria

0
220

Rais Samia Suluhu Hassan ametia saini miswada miwili ambayo ilipitishwa na mkutano wa saba wa Bunge na kuwa sheria kamili.

Akitoa taarifa ya Spika Bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amesema miswada hiyo sasa imekuwa sheria na tayari zimeanza kufanya kazi.

“Waheshimiwa Wabunge napenda kutoa taarifa kuwa miswada miwili ambayo imepitishwa na Bunge katika mkutano wa saba sasa imekuwa sheria kamili ambazo zinaitwa Sheria ya matumizi ya serikali namba 4 ya mwaka 2022 na sheria ya fedha namba 5 ya mwaka 2022.” amesema Spika