Rais ateua Mtendaji Mkuu mpya TANROADS

0
149

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mhandisi Rogatus Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) (Miundombinu).

Mhandisi Mativila alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Rais Samia pia amemteua Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Mhandisi Besta ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (CASSOA).

Kamishna Benedict Wakulyamba ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kamishna Wakulyamba anachukua nafasi ya Anderson Mutatembwa ambaye amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Amemteua Mhandisi Amin Mcharo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Uteuzi wa viongozi hao umeanza Juni 12, 2023.