Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali ambapo ametengua uteuzi wa Reuben Mfune, (Mkuu wa wilaya ya Mbarali), Msongela Palela (Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Musoma, Mara) na Michael Matomora (Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba, Singida).
Wengine ambao uteuzi wao umetenguliwa ni Linno Mwageni (Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Shinyanga) na Sunday Ndori (Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa, Njombe).
Uteuzi wa viongozi hao ulitenguliwa kuanzia tarehe 22 mwezi huu.