Rais atengua uteuzi wa Azza Hamad, ateua mrithi

0
528

Rais Samia Suluhu Hassa ametengua uteuzi wa Azza Hilal Hamad aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu.

Bi. Azza atapangiwa majukumu mengine.

Kufuatia uamuzi huo, Rais Samia amemteua Bi. Prisca Joseph Kayombo kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu.

Kabla ya uteuzi huo Kayombo alikuwa Afisa Mkuu wa Utawala na Utumishi katika Wizara ya Fedha na Mipango na ataapishwa pamoja na Makatibu Tawala wengine siku ya Jumatano Juni 2, 2021 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.