Rais arejea kutoka Maputo

0
188

Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali alipowasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma leo, akitokea Maputo nchini Msumbiji kuhudhuria mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Wakati wa mkutano huo SADC imeridhia kuanzishwa kwa Kituo cha Haki za Binadamu kitakachosaidia nchi zinazokabiliwa na athari za mabadiliko ya Tabia Nchi, kukabiliana na janga la corona pamoja na kuangalia jinsi gani SADC itaweza kupambana na suala la ugaidi.