Rais aomboleza waliofariki kwenye ajali

0
154

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa na vifo vya watu 22 vilivyotokea baada ya basi kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Melela Kibaoni wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais amewapa pole wafiwa, amewaombea Marehemu wapumzike mahali pema na kwa majeruhi amewaombea wapone haraka.

Pia amewasihi watumiaji wa barabara kuzingatia sheria za barabarani.