Rais aomboleza vifo vya waliofariki kwenye ajali Iringa

0
154

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa, Queen Sendiga kufuatia vifo vya watu 19 vilivyotokea kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea alfajiri ya leo kwenye eneo la Changarawe, Mafinga mkoani humo.
 
Pia amewapa pole wafiwa wote na kusema kuwa anaungana na familia zilizopoteza wapendwa wao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
 
Katika  salamu zake, Rais Samia Suluhu Hassan amevitaka vyombo vinavyosimamia usalama barabarani kuendelea kutoa elimu kwa madereva ili wazingatie sheria za usalama barabarani.