Rais amedhamiria kumtua mwanamke kuni

0
173

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana amesema
uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuibeba kwa uzito ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia unadhihirisha umakini, uwezo na nia yake safi ya kuwainua wanawake kiuchumi.

Kinana amesema kampeni ya Nishati Safi iliyoanzishwa na Rais Samia inalenga kumtua mwanamke mzigo wa kuni kichwani na kumpa muda mwingi wa kujikita katika shughuli za kujiletea maendeleo.

Kinana ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika Kata ya Ngerengere Halmashauri ya Morogoro Vijijini.

“Nimeona mitungi ya gesi ambayo nitaikabidhi, na uwepo wa mitungi hii ni matokeo ya sera na ubunifu kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mwaka jana Rais Samia alianzisha mchakato wa kuwatua akina mama mzigo wa kuni, kaanzisha mradi wa nishati safi na salama”. Amesema Kinana