Rais akagua ujenzi mwendokasi

0
381

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya ziara ya kushtukiza kukagua awamu ya pili ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi unaofanyika kutoka eneo la Kariakoo hadi Mbagala, katika eneo la Mtoni Mtongani mkoani Dar es salaam.

Akizungumza na Wakazi wa eneo hilo mara baada ya ukaguzi huo, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, Serikali itahakikisha ujenzi wa barabara hiyo unakamilika katika muda uliopangwa ili kuwarahisishia usafiri Wakazi wa maeneo hayo.

Amesema Serikali itashughulikia changamoto zote ambazo zitaonekana kuwa ni kikwazo katika ujenzi wa barabara hiyo.

Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kurejea katika eneo hilo  siku chanche zijazo, kwa lengo la kukagua tena maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.

Ameeleza kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo, ambao kwa sasa umefikia asilimia 16.