Rais aishukuru familia ya Mwalimu Nyerere
Rais Samia Suluhu Hassan, ameishukuru familia ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwa mstari wa mbele katika kutetea na kupigania maslahi ya nchi.
Rais Samia ameyasema hayo alipozuru kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mapema leo wilayani Butiama na kisha kupata fursa ya kuongea na familia hiyo.
Rais ameiambia familia hiyo kuwa, Baba wa Taifa pamoja na baadhi ya viongozi katika familia hiyo walifanya mambo makubwa ya kiukombozi yaliyopelekea Taifa kujipatia uhuru, hivyo jitihada hizo ni za kuenziwa.
Ameongeza kuwa Taifa linajivunia kuwa na familia kama hiyo na litaendelea kuithamini kwa mchango huo,
Rais Samia anamaliza ziara yake mkoani Mara kwa kuzungumza na Wananchi wa Bunda mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chujio la maji, Mradi wa Maji Maji Bunda.