Rais afanya uteuzi na uhamisho wa viongozi

0
226

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko kwa baadhi ya viongozi kwa kuteua Waziri na Naibu Waziri, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu wakuu wa wizara na kuwahamisha wizara baadhi ya viongozi.

Rais pia amemteua Ramadhani Kailima kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Uapisho wa viongozi hao utafanyika saa 10 jioni, Jumatatu Februari 27, 2023 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.