Rais afanya mabadiliko madogo kwa Ma-RC

0
178

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo kwa baadhi ya wakuu wa mikoa ambapo amemteua Said Mtanda kuwa mkuu wa mkoa wa Mara.

Kabla ya uteuzi huo Mtanda alikuwa mkuu wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora na anachukua nafasi ya Meja Jenerali Suleiman Mzee ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Pia amemuhamisha Queen Sendiga kuwa mkuu wa nkoa wa Manyara akitokea mkoa wa Rukwa.

Sendiga anachukua nafasi ya Charles Makongoro Nyerere ambaye amehamishiwa mkoa wa Rukwa.

Kenani Kihongosi ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Urambo na anachukua nafasi ya Said Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara.

Uteuzi huo umeanza mara moja.