Rais Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini jioni ya leo kuelekea Ufaransa na baadaye Ubelgiji kwaajili ya ziara ya kikazi katika nchi hizo.
Aidha, akiwa nchini Ufaransa, Rais Samia anatarajia kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari duniani.
Pia, Rais Samia atashuhudia utiaji saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa katika sekta za miradi ya maendeleo, ushirikiano katika masuala ya uchumi wa buluu, usalama wa bahari, sekta ya usafiri na maendeleo endelevu.
Rais amesindikizwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango pamoja na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume Zanzibar kabla ya kuondoka kuelekea Ufaransa leo.
Katika hatua nyingine Rais anatarajiwa kuzungumza na Watanzania wanaoishi nchini Ufaransa.