Rais aagiza Polisi kumuachia Mkuu wa Shule iliyoungua moto Kagera

0
239

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli ameliagiza Jeshi la polisi mkoani Kagera kumuachia huru Mkuu wa Shule ya Islamic Byamungu, anayeshikiliwa baada ya wafunzi 10 kufariki dunia na 7 kujeruhiwa kwa moto ulioteketeza bweni la wavulana.

Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo leo Septemba 16, 2020 akiwa Kagera katika mwendelezo wa kampeni zake za urais.

“Nafahamu Mkuu wa Shule iliyoungua Kyerwa ameshikiliwa na Polisi, ningeomba polisi wakati uchunguzi unaendelea mkuu wa shule wamuachie ili wadhibiti na kujua kama ilikuwa ni ajali kweli au palikuwa na uzembe,hata akiwa nje atashirikiana na Polisi, ” amesema Rais Magufuli.