Raia wa Kenya zaidi ya 1,400 waliopo nchini wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, kwenye vituo vitatu vilivyoandaliwa hapa nchini.
Msimamizi wa uchaguzi mkuu wa Kenya katika kituo cha ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini Samwel Mwangi amesema, raia zaidi ya 900 wa nchi hiyo watapiga kura katika vituo viwili vilivyopo kwenye ubalozi wa Kenya uliopo mkoani Dar es Salaam.
Amesema mbali na vituo hivyo viwili vilivyopo Dar es Salaam, raia wengine wa Kenya wanatarajiwa kupiga kura katika kituo kilichopo jijini Arusha.
Uchaguzi Mkuu wa Kenya umepangwa kufanyika tarehe 9 mwezi huu.