Qatar yaahidi kuipiga tafu Taifa Stars

0
307

Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Hussain Ahmad Al – Homaid ameahidi kutoa ushirikiano kwa serikali katika kuiwezesha timu ya taifa ya Tanzania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini humo.

Balozi huyo ametoa ahadi hiyo kufuatia ombi la Waziri wa Habari, Innocent Bashungwa ambaye ameliomba taifa hilo kuisaidia timu ya Taifa katika maandalizi yake ya michuano ya kushiriki mashindano hayo makubwa zaidi duniani.

Bashungwa ametoa ombi hilo katika kikao kilichokuwa na lengo la kuona namna Qatar itakavyoweza kusaidia tasnia ya filamu nchini, masoko kwa sanaa za ufundi, uendelezaji wa viwanja vya michezo pamoja na kubadilishana uzoefu katika sekta ya habari.

Taifa Stars ina michezo kadhaa mkononi katika kuwania kufuzu mashindano hayo.