PSSSF yawatahadharisha Wanachama wake kuhusu matapeli  

0
179

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesisitiza kuwa huduma zinazotolewa na mfuko huo ni bure, hivyo Wanachama hawapaswi kulipa gharama zozote pindi wanapohitaji huduma kutoka kwenye mfuko huo.

Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Elimu kwa Umma wa PSSSF, Eunice Chiume ametoa kauli hiyo kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa, kuna baadhi ya watu wasio waaminifu ambao wamekua wakiwapigia simu Wastaafu wa PSSSF na kuwataka wawatumie fedha kwa ajili ya fomu, Vat na Stamp Duty ili waweze kulipwa malipo yao.