Profesa Mohamed Khalfan bosi mpya PDB

0
326

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Profesa Mohamed Hafidh Khalfan kuwa mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (PDB)

Kabla ya uteuzi huo Profesa Khalfan alikuwa Mhadhiri Huria katika Taaluma, Ushauri Elekezi na Utafiti.

Ofisi ya PDB imeanzishwa na Dkt. Mwinyi ili kufuatilia utekelezaji wa miradi na mikakati mbalimbali ya Serikali iwe na ufanisi na kukamilika kwa wakati.