Profesa Elisante awafunda makandarasi

0
169

Makandarasi wazalendo wanaosimamia miradi ya mahakama kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa ili kuwezesha upatikanaji wa haki inatolewa kwenye mazingira bora.

Rai hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa mahakama Profesa Elisante Ole Gabrieli wakati wa kikao chake na makandarasi wa miradi ya mahakama kilichofanyika Kituo Jumuishi cha Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Profeaa Elisante amesema, mpaka sasa mahakama ina miradi 34 inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini na imewaamini wakandarasi wa ndani kufanya kazi katika miradi hiyo, hivyo watumie fedha watakazopatiwa kwa matumizi sahihi.

“Tuna Mahakama za Mwanzo 960, Mahakama za Wilaya 120, Mahakama za Hakimu Mkazi 30, Mahakama Kuu 18 na Rufani lakini pia tuna vituo vya kutolea huduma sita katika Mikoa mitano na ujenzi unaendelea,” amesema Profesa Gabriel.

Amesema, lengo kubwa kutumia makandarasi wa ndani ni kuwakuza katika kazi zao hivyo, wanapaswa kuongeza kasi ya utendaji na utaalamu.

Aidha, amewataka wakandarasi hao kuwa imara kifedha kwa sababu upatikanaji wa fedha serikalini unahitaji mchakato hivyo, wasisubiri fedha ndipo waanze ujenzi badala yake waendelee na ujenzi na wakati wakisubiri kulipwa fedha zao