Watawala wa Cambridge na Sussex wametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha babu yao, mtawala wa Edinburgh Prince Philip
aliyefariki dunia ijumaa iliyopita nchini Uingereza akiwa na umri wa miaka 99.
Katika salamu zao walizozitoa kwa nyakati tofauti, Prince William amemtaja Prince Philip kuwa alikuwa ni mtu wa kipekee.
Naye Prince Harry amemuelezea babu yake kuwa alikuwa mtu wa kujitoa kwa ajili ya wengine na alikuwa ni mwenye busara.
Mazishi ya Prince Philip yatakayofanyika tarehe 17 mwezi huu huko St George’s Chapel, katika uwanja wa jumba la Windsor ambapo Prince William na Prince Harry watakutana katika mazishi hayo.
Habari zaidi zinaeleza kuwa mazishi hayo yatatangazwa moja kwa moja na vituo mbalimbali ya televisheni duniani.