Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Pauline Gekul, amelipongeza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupitia TBC FM, kwa kuandaa tuzo kwa Wanafunzi wa uandishi wa habari na utangazaji na kutilia mkazo suala la maadili na utamaduni.
Naibu Waziri Gekul, amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatilia mkazo maadili na utamaduni, hivyo anaipongeza TBC kwa kuliona hilo na kuvisihi vyombo vingine vya habari nchini kuiga jambo hilo.
“Nawapa pongezi kwa hizi tuzo, Serikali inafarijika kuona maadili na utamaduni yanatiliwa mkazo, na hili hata Rais Samia Suluhu Hassan analitilia mkazo kwa hiyo nawapongeza sana.” Amesema Gekul
Naibu Waziri Gekul ni mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa Wanafunzi wa uandishi wa habari na utangazaji, hafla iliyoandaliwa na TBC.