Polisi Ruvuma atuhumiwa kujeruhi Raia kwa wivu wa kimapenzi

0
246

Jeshi la Polisi la mkoani Ruvuma linamshikilia askari wake aitwaye Pc Keneth Mkwela kwa kosa la kumjeruhi Andrew Milanzi mwenye umri wa miaka 33 kwa kutumia kitu chenye ncha kali kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma, – Pili Mande amesema tukio limetokea katika Kijiji cha Magagula wilaya ya Songea kwenye nyumba ya wageni baada ya askari huyo kubaini Milanzi alikuwa akifanya mawasiliano na mwenza wake.

Amesema inadaiwa kuwa askari huyo alimchoma raia huyo na kitu chenye ncha kali katika eneo la chini ya ubavu wa kushoto na kumsababishia mjeruhiwa huyo maumivu makali ambayo yamesababisha kulazwa katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma.

Polisi mkoani Ruvuma wanaendelea kumshilikilia askari huyo wakati akisubiri taratibu za kisheria pamoja na taratibu za kiaskari katika kipengele cha nidhamu ya askari.