Polisi kuweni mabalozi wa elimu ya fedha

0
142

Polisi wilayani Missenyi mkoani Kagera wametakiwa kuwa mabalozi kwa wananchi wanaowazunguka ili kuwafikishia elimu ya masuala ya fedha waliyoipata kutoka kwa timu ya wataalamu wa Wizara ya Fedha iliyoko katika kampeni ya kutoa elimu ya fedha kwa umma kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Missenyi Jonas Soa wakati akizungumza na askari Polisi katika semina iliyofanyika kwenye Viwanja vya Kituo Cha Polisi Kyaka.

“Tunaahidi kuwaelimisha Polisi wengine ambao hawajapata elimu hii, lakini pia tutawajengea uwezo Polisi Jamii ili wawaelimisha wananchi ambao wapo karibu nao waepukanane na mikopo umiza”.Amesema Soa

Ameongeza kuwa elimu ikiwafikia wananchi wote itaisaidia kupunguza migogoro ambayo imekuwa ikifikishwa kwenye vituo vya Polisi kuhusu mikopo umiza ambayo imekuwa kero kwa wananchi.