Polisi kufanya uchunguzi gharama za matibabu Hospitali ya Aga Khan

0
211

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefungua jalada la uchunguzi kwa Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kutozwa gharama kubwa za matibabu kwa wagonjwa wa matatizo ya kifua (Pneumonia).

Malalamiko hayo kutoka kwa wananchi pia yamebainisha kuwa, wagonjwa wanaopatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo pindi wanapofariki dunia, miili yao huzuiwa na kudai kiasi kikubwa cha fedha kinyume na maelekezo ya serikali kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.

Jeshi hilo kupitia kwa Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema, uchunguzi utakapokamilika na kubaini tuhuma juu ya hospitali hiyo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limefanikiwa kuwaua majambazi na kukamata silaha aina ya Shortgun ikiwa na risasi mbili ndani ya kasha.