Polisi anayenyanyasa raia kukiona

0
253

Serikali imesema itamchukulia hatua za kisheria askari polisi  atakayebainika kufanya vitendo vya unyayasasi dhidi ya watu wanaowakamata kwa tuhuma mbalimbali.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.Kangi Lugola amesema kutokana na uwepo wa malalamiko dhidi ya baadhi ya askari kudaiwa kuwatesa wananchi kwa makusudi atafanya ziara nchi nzima kubaini ukubwa wa tatizo hilo