Poland kuisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali

0
229

Rais Andrzeja Duda wa Poland amesema nchi yake ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Viwanda vya Kilimo na uzalishaji kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Rais Duda pia ametoa fursa kwa Vijana wa Kitanzania kwenda Poland kupata elimu kuhusiana na mambo mbalimbali ambayo kwao wamepiga hatua kubwa ikiwemo teknolojia ya kuchimba madini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza mazungumzo baina yake na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu, Dar es Salaam Rais Duda amesema, nchi yake itaendeleza ushirikiano na Tanzania ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 62 kwa kuwekeza zaidi hapa nchini.

Amesema Poland itawashawishi Wawekezaji zaidi ambao wengine wapo tayari Barani Afrika kuwekeza hapa nchini ili kuongeza tija kwenye malighafi zinazopatikana Tanzania.

Ziara hiyo ya Kitaifa ya siku mbili ya Rais Duda nchini imehitimishwa hii leo na ametoa mwaliko kwa Rais Samia Suluhu Hassan kufanya ziara ya Kitaifa nchini Poland.