Pingamizi shauri la Mbowe lawasilishwa

0
143
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akizungumza na wandishi wa habari, bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman

Upande wa Jamhuri umewasilisha pingamizi dhidi ya shauri la kikatiba lililofunguliwa na Mwenyekiti Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe dhidi ya Serikali.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa ufunguzi wa kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mbowe dhidi ya Serikali umekiuka baadhi ya vipengele vya kisheria, hivyo kuomba mahakama kutupilia mbali shauri hilo.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo ya pingamizi iliyowasilishwa na wakili wa Serikali Mkuu Hangi Chang’a, Jaji wa Mahakama Kuu John Mgeta umeutaka upande wa Serikali kuwasilisha hoja za pingamizi kimaandishi Septemba 6 mwaka huu na ule upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala ukitakiwa kuwasilisha hoja zao kimaandishi Septemba 9 mwaka huu.

Katika kesi ya Msingi Freeman Mbowe kupitia kwa Wakili wake Kibatala anadai kuvunjwa kwa matakwa ya kikatiba wakati wa kukamatwa na kushtakiwa kwake kwa makosa ya ugaidi.

Katika hati ya mashtaka, wanaoshtakiwa na upande wa utetezi ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Siro na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 23 mwaka huu kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Upande wa Jamhuri umewasilisha pingamizi dhidi ya shauri la kikatiba lililofunguliwa na Mwenyekiti Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe dhidi ya Serikali.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa ufunguzi wa kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mbowe dhidi ya Serikali umekiuka baadhi ya vipengele vya kisheria, hivyo kuomba mahakama kutupilia mbali shauri hilo.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo ya pingamizi iliyowasilishwa na wakili wa Serikali Mkuu Hangi Chang’a, Jaji wa Mahakama Kuu John Mageta umeutaka upande wa Serikali kuwasilisha hoja za pingamizi kimaandishi Septemba 6 mwaka huu na ule upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala ukitakiwa kuwasilisha hoja zao kimaandishi Septemba 9 mwaka huu.