Picha: Jionee uzuri wa Njia ya Marangu kupanda Ml. Kilimanjaro

0
331

Baada ya Njia ya Marangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro kushinda tuzo kutoka nchini China kwa kutambuliwa kuwa njia bora zaidi ya kupanda kwenye mlima huo, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limefunga safari na kuikagua na kukuza uelewa kuhusu njia hiyo.

Tazama picha mbalimbali za safari hiyo kuelekea Kituo cha Mandara.

Kabla ya safari tukajifunza mawili matatu kuhusu Mlima Kilimanjaro.
Safari ni hatua, na hapa timu imepo tayari kufuta vilima vya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro hadi Kituo cha Mandara (8km).

Watumishi wa TBC wakiendelea kufuta vilima kuelekea kituo cha Mandara
Kula ni muhimu ili kuupa mwili nguvu. Zingatia, uchafu wote unatakiwa kuutupa kwenye maeneo maalum.
Kupanda mlima sio vita, ni burudani, tabasamu ni muhimu katika safari.
Sauti za maji ni za kuliwaza pindi uzisikiapo ukiendelea kupanda Mlima.
Unapopanda Mlima kuna maeneo maalum yametengwa kwa ajili ya kupumzika na kula
Kunywa maji ni muhimu, kabla na wakati wa kupanda mlima. Watalii hawaruhusiwi kuingia hifadhi wakiwa na chupa za maji ambazo zinatumika mara moja (non-reusable).
Majadiliano yakiendelea wakati wa kupanda mlima
Hisia mbalimbali zitaonekana katika safari. Wapo watakaokuwa na nyuso za huzuni kwa kuchoka, wengine watakuwa na furaha, kikubwa safari itasogea.
Wanyama na ndege mbalimbali wamepamba Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro
Shughuli za kurekodi matukio nazo hazikosekani. Utawambia nini watu kama hutapost picha?
Safari
Uchovu ukikukamata, basi unataka kujigeuza kuwa mti
Watalii mbalimbali wakipanda Mlima Kilimanjaro
Walioitwa ni wengi, ila wateule ni wachache. Wateule wakiwa katika kituo cha Mandara, ambacho ni kituo cha kwanza wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro
Kuna baridi, sio kesi, push-ups mbili tatu kupasha mwili joto katika Kituo cha Mandara
Shunguli ya kuujuza umma kuhusu uzuri wa Tanzania ukiendelea kutoka kwa watumishi wa TBC.

Uzuri, upekee na mvuto wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, na Njia ya Marangu, haviwezi kuwekwa kwa 100% kwenye picha. Unashauriwa kutenga muda kutembelea hifadhi hiyo na vivutio vingine, kuweza kuyaona hayo na mengine mengi.