Petroli, dizeli bei juu kuanzia kesho

0
248

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza ongezeko la bei ya mafuta kuanzia hapo kesho.

Mkurugenzi wa Petroli wa EWURA Gerald Maganga amesema bei mpya ya petroli kwa mafuta yanayopokelewa kupitia bandari ya Dar es salaam itakuwa shilingi 2,861 kutoka shilingi 2,540, ikiwa ni ongezeko la shilingi 321.

Kwa upande wa dizeli bei mpya itakuwa shilingi 2,692 kutoka shilingi 2,403 ya sasa, ikiwa ni ongezeko la shilingi 289.

Mafuta ya taa bei itapanda kutoka 2,208 hadi shilimgi 2,682.

Mkurugenzi huyo wa Petroli kutoka EWURA amewaambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa mafuta ambayo yatapitia bandari ya Tanga, bei ya petroli itakuwa shilingi 2,848 kutoka shilinhi 2,563 ikiwa ni ongezeko la shilingi 285.