Paspoti ya Tanzania yaingia kumi bora barani Afrika.

0
312

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2020 iliyotolewa na Henley & Partners nchi 10 zinazoongoza duniani kwa kuwa na paspoti imara zaidi ni Japan, Singapore, Ujerumani, Korea Kusini, Finland, Italy, Denmark, Luxembourg, Uhispania, na Ufaransa.

Kwa upande wa Afrika, Tanzania imeshika nafasi ya 73 duniani huku ikiwa katika nafasi ya 10 barani Afrika kwa uimara wa paspoti.

Nchi za Africa zenye paspoti imara zaidi (kwenye mabano ni nafasi zao katika orodha ya dunia) ni:

??Shelisheli (29)
??Mauritius (32)
??Afrika Kusini (56)
??Botswana (62)
??Namibia (67)
??Lesotho (69)
??eSwatini (70)
??Malawi (71)
??Kenya (72)
??Tanzania (73)

Wakati huo huo, Idara ya Uhamiaji nchini imesema mpaka Desemba 31 mwaka jana, jumla ya Watanzania 237,946 walikuwa wamepata paspoti mpya ambapo kati yao, wananchi wa kawaida ni 237,813 , huku 459 zimetolewa kwa viongozi wakuu waandamizi wa Serikali, 1,672 zimetolewa kwa wenye hadhi ya kidiplomasia na tano ni za viongozi wakuu wa nchi.