Orodha ya washindi wa tuzo za Uandishi wa Habari Mbeya

0
116

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye usiku wa Januari 7, 2023 alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (Tulia Trust Journalism Awards) 2022/23 jijini Mbeya.

Waandishi walioibuka kidedea katika tuzo hizo ambazo lengo kuu ni kuchochea hamasa ya vyombo vya Habari pamoja na Wanahabari kufanya kazi zao katika weledi ni;

Ezekiel Kamanga
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Madini na Gesi (Online TV)

Rashid Mkwinda
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Online TV)

Enock Simon
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Watoto (Online TV)

Joseph Mwaisango
Tuzo ya Mpigapicha Bora (Online TV)

Joseph Mwaisango
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Maliasili (Online TV)

Kakuru Msimu
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utamaduni na Michezo

Joseph Mwaisango
Tuzo ya Mshindi wa Jumla (Online TV)

Kwa upande wa vituo vya redio:

Samwel Mussa, Pascal Ndambo na Fredrick Gumusu
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya ni

Esther Lekasio na Joshua Sengo
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Mazingira

Jirani Mtembezi na Samwel Mussa
Tuzo ya Habari za Michezo

Prince Fungo
Tuzo ya Habari za Uchumi na Biashara

Anitha Mahenge
Tuzo ya Uandishi wa Habari za Unyanyasaji wa Kijinsia

Isakwisa Mbyale na Joshua Sengo
Tuzo ya Habari za Watoto.

Wakati huohuo taasisi ya Tulia Trust ikiongozwa na Mkurugenzi wake Dkt. Tulia Ackson ilitoa mchango wa shilingi milioni 15 kwa Umoja wa Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya (Mbeya Press Club Vikoba) kama sehemu ya kuwaongezea mtaji wa kukopeshana kwenye mfuko wao.