Ongeza matumizi ya zabibu

0
90

Kilimo cha zabibu kwa Tanzania kimeshika kasi mkoani Dodoma, ambapo ndio kitovu cha zao hili lenye matumizi mengi na faida za kipekee sana.

Wengi hula zabibu bila kujua faida zake huku wengine wakidhani zabibu hutumika kutengeneza mvinyo pekee.

Wataalamu wa afya wanashauri mtu kula zabibu kwa wingi kutokana na matunda haya kuwa na virutubisho vingi kwa ajili ya kinga ya mwili na afya bora.

Matunda haya yana vItamini B1, B2, B6, C, E, K, protini, potasiamu na madini mengine mengi.

Zabibu husaidia kulinda afya ya moyo kutokana na potasiamu ambayo husaidia kupunguza tatizo shinikizo la chini la damu na kuuweka sawa mzunguko wa damu.

Zabibu ina virutubisho ambavyo hupambana na saratani. Matunda haya yana misombo yenye ‘antioxidants’ yaani misombo ambayo husaidia kurekebisha uharibifu wa seli. Antioxidants kama Resveratrol hupunguza uvimbe na kusambaa kwa seli za saratani.

Quercetin, anthocyanin na catechin nazo pia zina nguvu ya kupigana na seli zinazosababisha saratani.

Ni kinga dhidi ya kisukari. Japo zabibu huwa na sukari nyingi zinaweza kuongeza viwango vya sukari kwenye damu kwa kasi kidogo au wastani bila kusababisha kisukari.