Aliyekuwa Waziri Mkuu nchini Kenya Raila Odinga hii leo amezitembelea familia za marais wa zamani nchini Tanzania Hayati John Pombe Magufuli na ile ya Benjamin Mkapa.
Raila ambaye hapo Jana alishudhuria sherehe za kumuapishwa rais mpya wa Zambia Hakainde Hichilema alipiga picha na wake za marais hao wawili wakiwa nyumbani kwao.
Katika chapisho lake la twitter Raila amesema: ‘’Nimepitia ili kutembelea familia za rafiki zangu rais Benjamin Mkapa na John Magufuli. Nafurahia kukutana na Anna Mkapa na Janeth Magufuli wakiwa katika hali nzuri’’.
Baadaye alimaliza kusema: “Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi….” Kiongozi huyo amekuwa rafiki wa karibu wa viongozi hao wawili waliofariki na hususan John Pombe Magufuli kabla na hata alipokuwa rais wa Tanzania na haitmaye kifo chake.