Nyerere aliweka sera madhubuti ya Mambo ya Nje

0
190

Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali mstaafu Ludovic Utoh amesema chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Tanzania ilikuwa na sera madhubuti ya Mambo ya nje na kuifanya ifahamike zaidi ulimwenguni.

Utoh ametoa kauli hiyo wakati wa kongamano la kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mwalimu Nyerere linalofanyika katika Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es salaam.

Amesema kuwa enzi za vita baridi kati ya mataifa ya Magharibi na yake ya Mashariki Tanzania haikua na upande wowote na hivyo kubakia Taifa lenye kuwa na msimamo unaojitegemea.

Ameongeza kuwa, sera zilizowekwa na Mwalimu Nyerere miaka ya 60 ndio ambazo mpaka sasa zinaifanya Tanzania kuheshimika kimataifa.