Nyani bado tishio Wilaya ya Rombo

0
170

Waziri wa Kilimo Profesa Adolph Mkenda amesema bado suala la uwepo wa nyani katika wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro imekuwa ni changamoto hasa katika vijiji vilivyoko ukanda wa juu.

Profesa Mkenda ameyasema hayo wilayani Rombo wakati akizungumnza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa licha ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuingilia kati suala hilo lakini bado ni tatizo.

Amesema uwepo wa nyani hao umechangia mazao ikiwemo ndizi kuliwa pamoja huku usalama wa watoto kuwa hatarini.

Nao baadhi ya viongozi wa vijiji vinavyozungumza msitu wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro wamesema kwa sasa wananchi wamekuwa wakiishi kwa hofu kwani nyani hao wamekuwa wakifika katika makazi yao muda wote.

Wamesema wazazi wqnalazimika kuwa karibu na watoto wao muda wote kwani nyani wamekuwa wakiwajeruhi pindi wanapofika katika makazi yao.

Vijiji vya Mrere, Kirwa na Katangara ni baadhi ya vijiji ambavyo vimeathiriwa na uwepo wa nyani hao.