Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Oktoba 01, 2022 ameongoza mbio za hisani za Benki ya NMB (NMB Marathon) jijini Dar es Salaam, za kuchangia matibabu ya wanawake wenye tatizo la Fistula.
Kupitia mbio hizo shilingi milioni 600 zimepatikana kwa ajili ya kugharamia matibabu ya ugonjwa huo.
Mbio hizo zilianzia katika viwanja vya Leaders Club, kuzunguka katika viunga vya jijini hilo na kuishia katika viwanja hivyo.