Mkuu wa mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amesema mkoa huo tayari unekamilisha zoezi la sensa ya watu na makazi.
Mtaka ameyasema hayo wilayani Makete alipofika kukagua zoezi hilo, ikiwa ni wilaya mwisho kufanya ukaguzi huo.
Mkuu wa wilaya ya Makete, Juma Sweda amesema kazi inayofanywa kwa sasa na makarani wa sensa ni kuhakiki kwa kupita kwenye kaya binafsi na jumuishi.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere amesema licha ya changamoto za mawasiliano na usafiri kutokana na jiografia ya maeneo hayo, makarani wanachofanya hivi sasa ni kuingiza kwenye mfumo taarifa walizozikusanya.