Rais Samia Suluhu Hassan leo amemuapisha Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi pamoja na Waziri Kidamba kuwa mkuu wa mkoa wa Njombe.
Halfa ya kuwaapisha Polepole na Kidamba imefanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali.
Akizungumza baada ya kuwaapisha Viongozi hao Rais Samia Suluhu Hassan amesema atakutana na Balozi Polepole na kuzungumza naye kirefu kabla hajaelekea nchini Malawi.
Kwa upande wa Kindamba ambaye ameapishwa kuwa mkuu wa mkoa wa Njombe amemtaka kwenda kuangalia suala la lishe pamoja na kuhamasisha chanjo ya UVIKO – 19 katika mkoa huo.
Kabla ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Polepole alikuwa Mbunge wa kuteuliwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kidamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).