Nitawaongezea Jimbo la Kawe makatapila 20

0
348

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amesema amesikia kero za wananchi wa Jimbo la Kawe hasa kwenye suala la barabara na kuamua kumuunga mkono Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima katika kutengeneza barabara hizo kwa kuahidi kutoa makatapila 20 ndani ya wiki moja ili ziweze kusaidia kutengeneza barabara zote zilizoharibika.

Akizingumza katika ziara ya kichama katika kiwanja cha shule ya Bunju, Dar es Salaam, Makonda amesema yupo kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi na sio kubeba ahadi yoyote. Amesema “wakati nakuja niliuliza kati ya changamoto kubwa ni nini, nikaambiwa ni barabara. Mimi siyo wa kubeba ahadi ni wa kutekeleza.”