Nishati chafu yasababisha vifo Mil 2

0
145

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amesema zaidi ya watu Milioni mbili hufariki dunia kila mwaka duniani kote kutokana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia.

Jafo amesema hayo leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam ambapo imefanyika hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024 – 2034.

Amesema matumizi ya nishati chafu yameleta athari kubwa katika jamii, ambapo akina mama ndio waathirika wakubwa.

Aidha, Waziri Jafo amesema Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imejipanga vema kufanya usimamizi wa utunzaji wa mazingira kwa kusimamia shughuli mbalimbali ambazo zitasaidia suala zima la upelekaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi.