Nimewanunulia Kawe greda ya kuchonga barabara

0
429

Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima amesema ametimiza ahadi yake ya kununua greda kwa ajili kukarabati barabara kwenye jimbo hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Akizungumza katika kiwanja cha Shule Bunju wakati wa ziara ya Katibu wa NEC ya CCM- Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda, amesema ameishawishi Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni kununua greda ili washirikiane katika kutengeneza barabara na kutatua kero hizo.

Aidha, amemuomba Makonda awakilishe kero zao za barabara kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Samia Suluhu kuhusu changamoto za barabara na vivuko vilivyoharibika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.