“Mimi nilitoka hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari bila kushurutishwa wala kushawishiwa na mtu na nilipofika Msomera kila kitu nilichoahidiwa nakiri nimepata hadi hati miliki. Na mwaka jana nimenufaika, nimepanda mahindi na kuvuna magunia 35 kwa mara ya kwanza, kitu ambacho sijawahi kuvuna kati ya miaka 60 niliyoishi Ngorongoro,” Gidion Laizer, mkazi wa Msomera aliyehama kutoka hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari.