NEC YAVIASA VYOMBO VYA HABARI KUZINGATIA WELEDI

0
302

Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) imekemea tabia ya baadhi wa vyombo vya habari ambavyo vinatangaza taarifa za mchakato wa uteuzi wa wabunge na madiwani ambazo sio sahihi.

Dkt. Wilson Mahera, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema vipo vyombo vya habari ambavyo vimetangaza kupita bila kupingwa kwa baadhi ya wagombea jambo ambalo ni kinyume na kanuni za uchaguzi.

Aidha Dkt. Mahera ameongeza kuwa kwa sasa ni kipindi cha pingamizi kwa wagombea kitakachodumu hadi saa 10 jioni ambapo mpaka sasa hakuna kipingamizi chochote kwa walioteuliwa kugombea urais na makamu wa rais.